- 2,525 viewsDuration: 3:36Jioni ya leo, hali imesalia tete eneo la Transmara magharibi, ambako mtu mmoja ameuawa kwenye mapigano mapya yaliyozuka mpaka wa Nkaararo na Enoretet. Watu wengine zaidi ya kumi wanauguza majeraha ya mishale baada ya kujeruhiwa kwenye machafuko haya ya punde. Maafisa wakuu wa usalama eneo hilo wamefanya mkutano wa dharura na kuagiza operesheni ya kiusalama kwenye eneo la mpakani, kama Chrispine Otieno anavyotuarifu kutoka Transmara.