Serikali inachunguza ripoti kutoka Mandera, kuhusiana na uwepo wa wanajeshi wa Jubaland humu nchini. Waziri wa usalama wa taifa Kipchumba Murkomen, amesema asasi husika zinachunguza madai hayo na iwapo itabainika kwamba kweli wapo wanajeshi wa kigeni humu nchini, basi hatua zifaazo zitachukuliwa. Gavana wa kaunti ya Mandera Mohammed Adan Khalif, awali alithibitisha uwepo wa wanajeshi hao katika kaunti hiyo, huku akihimiza asasi za usalama kuchukua hatua za dharura kuepusha maafa na uharibifu.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive