- 162 viewsDuration: 1:29Huenda ndoto ya mwanafunzi Holyz Otieno mwenye ulemavu wa ngozi katika shule ya msingi ya sanandiki eneo bunge la Kabuchai kaunti ya Bungoma ikazimwa iwapo wahisani hawatajitokeza kumlipia karo. Kulingana na Holyz ambaye alifanya vizuri katika mtihani wa kjsea, changamoto ya kifedha imekuwa ikiathiri pakubwa masomo yake ambapo analazimika kusalia nyumbani kwa muda mrefu huku wenzake wakiendelea na masomo.