- 6,678 viewsDuration: 3:30Watu watatu zaidi akiwemo afisa wa polisi wamekamatwa kuhusiana na mauwaji ya Daktari wa akili Victoria Mutiso. Afisa huyo wa polisi alikamatwa na bastola ya mauwaji kupatikana baada ya operesheni na maafisa wa DCI katika kituo cha polisi cha Karinde eneo la Kikuyu. Maafisa wa upelelezi wamefichua kwamba afisa huyo ndiye aliyefyatua risasi tatu zilizosababisha kifo cha dkt Mutiso wiki iliyopita. Afisa wa cheo cha inspekta anayehusishwa pakubwa katika kufanikisha uhalifu huo ikiwemo kumkabidhi polisi muuwaji bastola yuko mafichoni na anasakwa na polisi.