- 5,600 viewsDuration: 1:30Shughuli ya upigaji kura nchini uganda zilianza asubuhi ya leo huku wapikakura millioni 21 na laki sita wakitarajiwa kufika debeni kupiga kura. Masanduku ya kupigia kura pamoja na vifaa vingine vya kupigia kura viliwasilishwa na mmafisa ya tume ya uchaguzi huku shughuli hiyo ikionekana kuanza kwa upole wapiga kura wachache wakifika kuanzia mwendo wa saa moja asubuhi. Hata hivyo ulinzi mkali umeshuhudiwa katika vituo vya kupigia kura huku asasi za usalama zikishika doria.uchaguzi wa uganda umezingirwa na ati ati, huku serikali ikionekana kuwanyanyasa wafuasi na viongozi wa upinzani baadhi ya wanaharakati wangali wanazuiliwa akiwemo aliyekuwa kiongozi wa upinzani kizza besigye.rais museveni anatafuta muhula wake wa saba mfululizo, naye mpinzani wake mkuu robert kyagulanyi maarufu bobi wine anampinga kwa mara ya pili debeni