Rais William Ruto ameagiza kila mtoto wa Kenya aliyefanya mtihani wa kitaifa wa gredi ya tisa-KJSEA aripoti shuleni kufikia kesho. Amesisitiza kuwa hakuna mwanafunzi anayepaswa kufukuzwa au kunyimwa nafasi shuleni kwa sababu ya kukosa karo, sare au mahitaji mengine ya kimsingi. Ingawa wanafunzi wengi bado hawajaripoti shuleni kuanza masomo gredi ya 10 hata baada ya muda uliowekwa na wizara ya elimu kukamilika, serikali inaamini kuwa itafanikisha mpito wa wanafunzi kwa asilimia 100 kwa kundi la kwanza la wanafunzi wa gredi ya 10.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive