- 2,388 viewsDuration: 2:15Rais William Ruto amemkosoa kinara WA chama Cha Wiper Kalonzo Musyoka kwa kile anasema ni kudhalilisha miradi yake ya maendeleo haswa mradi wa punde wa mtaji wa biashara Kwa vijana wa NYOTA Ruto, aliyeongoza hafla ya kuusambaza mtaji huo Kwa vijana Kutoka kaunti za Murang'a, Kirinyaga, Nyeri na Nyandarua katika uwanja wa kabiru-ini huko Nyeri, amemtaka Kalonzo kuwaeleza vijana alichowafanikishia alipohudumu kama Makamu wa Rais. Vile vile Rais ameendelea kuzitetea sera na miradi ya serikali yake, akiitaja kuwa mstari wa mbele kuwahakikishia vijana nafasi za kazi humu nchini, na Hata ughaibuni.