Rais wa chama cha wanasheria humu nchini Faith Odhiambo, anasema amebatilisha uamuzi wake wa kususia jukumu alilokabidhiwa kwenye jopo la wataalamu kuhusu kufidiwa kwa waathiriwa wa ghasia za maandamano ili kuhakikisha zaidi ya familia 100 zilizopoteza wapendwa wao zinapata haki. Akizungumza baada ya kuapishwa kwa jopo hilo, Odhiambo alisisitiza kuwa shughuli hiyo haipaswi kuishia tu kwa fidia bali inapaswa kufuatilia haki ili kuhakikisha waliohusika na vitendo vya kikatili wanachukuliwa hatua za kisheria. Na jinsi anavyotueleza mwanahabari wetu Abdiaziz Hashim, jopo hilo la wanachama 18 lililoteuliwa na rais Williama Ruto, sasa litaanza kutathmini madai ya familia zilizoathirika.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive