- 3,251 viewsDuration: 2:26Rais William Ruto sasa anasema muungano wa UDA na ODM lazima ushinde uchaguzi mkuu wa mwaka 2027, akisema itakuwa hatari kubwa iwapo upinzani utachukua hatamu za uongozi. Akizungumza alipokuwa akiongoza kongamano la viongozi wa muungano huo mjini Naivasha, Rais Ruto alieleza baadhi ya mafanikio ya serikali yake, akisema kuna mengi yanayojiri katika Ruwaza ya mwaka wa 2060, ambayo itazinduliwa Jumatano. Mwanahabari wetu Emmanuel Too yuko Naivasha na ameandaa taarifa ifuatayo.