- 253 viewsDuration: 1:28Kampuni ya mawasiliano ya Safaricom imezindua kampeni ya Pata More Kaunti ya Mombasa hii leo katika Bustani la Mama Ngina. Mamia ya wakaazi walijitokeza na kujishindia zawadi. Kulingana na kampuni ya Safaricom, kampeni hiyo imechochewa na kupanda kwa gharama ya maisha ikilenga kuwapa thamani zaidi wateja kupitia huduma na bidhaa za mawasiliano. Afisa Mkuu wa Biashara na Wateja Fawzia Al-Kimanthi akisema kampeni hiyo itapanua huduma za kidijitali hasa mashinani ambako changamoto ya simu za rununu za kidijitali imekuwa ikishuhudiwa.