- 1,465 viewsDuration: 3:46Serikali itaweka vituo vya karantini katika maeneo mbalimbali nchini ili kuzuia ugonjwa wa Ebola kuingia na kusambaa nchini. Katibu wa Afya ya Umma, Mary Muthoni, amesema kuwa kutengwa kwa wanaoshukiwa kuambukizwa virusi vya Ebola kutasaidia pakubwa kuzuia ugonjwa huo kusambaa. Ripoti zinaashiria kuwa visa vya ugonjwa wa Ebola katika Democratic Republic of the Congo vimefikia 452 baada ya watu 71 zaidi kuambukizwa na vifo 82 kuripotiwa. Nchini Uganda, maambukizi yamefikia 19 huku watu wawili wakifariki kutokana na Ebola.