- 425 viewsDuration: 1:38Afisa mkuu wa Bima ya afya ya jamii - SHA - Dkt.Mercy Mwangangi amesema kuwa SHA ingali inakabiliwa na changamoto za mabadiliko ya mfumo wa utoaji huduma za bima ya afya na ulaghai. Changamoto hizo zinatatiza utoaji huduma kwa zaidi ya watu milioni 32 waliosajiliwa kufikia sasa. aidha ulaghai katika SHA unahusisha vituo mbalimbali vya afya, maafisa wa SHA pamoja na baadhi ya wananchi. Waziri wa afya Aden Duale amesema kuwa zaidi ya shilingi bilioni 164 zimelipwa kwa hospitali mbalimbali kwa huduma za SHA huku fedha zilizokusanywa zikiwa ni shilingi bilioni 203.