Shirika la utangazaji humu nchini KBC limeorodheshwa miongoni mwa mashirka ya serikali yanaliyotia fora. Haya ni kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na kampuni ya Kenya Track Survey katika kaunti zote 47 mnamo mwezi huu wa Januari. Kwa mujibu wa utafiti huo, shirika la KBC limepanua upeperushaji wa vipindi vya humu nchini, kuimarisha utangazaji wake kidijitali na kuboresha jukumu lake la kutoa habari na kuelimisha umma.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive