- 1,719 viewsDuration: 55sTume ya huduma za mahakama imeanza mahojiano ya kujaza nafasi za majaji wa mahakama ya rufaa na mahakama kuu. Hatua hii ikiwa sehemu ya kuimarisha utendakazi wa idara ya mahakama kwa kuongeza nguvu kazi na uwezo wa kushughulikia mirundiko ya kesi mahakamani. Miongoni mwa wanaohojiwa ji mwenyekiti wa halmashauri ya utendakazi wa polisi na mwenyekiti wa zamani wa IEBC Isaac Hassan na wasomi wa vyuo kikuu Prof. Migai Akech, Dr Lucy Wanja Julius na daktari Joseph Arimba Kaberia.