- 1,382 viewsDuration: 1:31Shughuli za uchukuzi na biashara zimeathirika pakubwa katika mji wa mpakani wa Busia hii leo, abiria na wafanyabiashara wakipungua maradufu kufuatia uchaguzi unaoendelea katika nchi jirani ya Uganda. Mabasi ya masafa marefu yamesalia kuegeshwa katika steni ya magari mjini Busia, abiria wengi kutoka nchi jirani ya Uganda na mataifa mengine jirani wakikosa kusafiri kama ilivyo kawaida. Mpaka huo umesalia na shughuli chache licha ya Alhamisi kuwa siku ya soko kubwa.