- 235 viewsDuration: 1:57Vijana kutoka kaunti sita za pwani wamefanya mkutano huko mombasa na kuhusishwa katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo pamoja na mazungumzo yanayolenga umoja wa taifa. Wakizungumza baada ya kikao hicho cha faragh huko nyali wametaka mradi wa nyota kuwafaidi vijana wote nchini na kuwataka wale waliopokea fedha hizo kuhakikisha wamezitumia ili kujinufaisha kibiashara. Aidha wametaka vijana kuwa katika meza ya mazungumzo ya kitaifa ili kuhakikisha matakwa ya vijana yametiliwa maanani hasa katika uundaji wa sera.