Skip to main content
Skip to main content

Viongozi wa Bomet wataka mazungumzo ya kitaifa kuhusu misukosuko shuleni

  • | Citizen TV
    582 views
    Duration: 1:54
    Viongozi kutoka kaunti ya Bomet wanataka washikadau wote kwenye sekta ya elimu waitishe mazungumzo ya dharura baina ya wanafunzi,walimu na wazazi kuhusiana na ongezeko la visa vya migomo katika shule mbalimbali nchini. Wakiongozwa na mbunge wa Bomet kati Richard Kilel,viongozi hawa wanasema kuwa jukumu la urekebishaji wa tabia za wanafunzi si mzigo wa walimu pekee ila wazazi pia lazima wahusishwe. Hata hivyo viongozi hawa wanasisitiza kuwa mbinu ya kutumia mazungumzo iwe njia ya kuleta maelewano baina ya wanafunzi na walimu ili kuepukana na machafuko shuleni.