- 4,999 viewsDuration: 2:58Viongozi wa serikali jumuishi sasa wanasema walitahadharisha baadhi ya viongozi wa upinzani kuhusu tabia ya kiongozi wa DCP Rigathi Gachagua kwamba ni mwenye siasa za migawanyiko wakisema muda ungalipo kwa naibu kiongozi wa chama cha Jubilee Dkt Fred Matiangi kurejea serikalini ili kufanya kazi na rais William Ruto.Wakizungumza huko Nyamira, Kakamega na Teso, katika hafla mbalimbali za kusaidia vikundi, wamesema kuwa wana uhakika kwamba Rais William Ruto atawabwaga wapinzani.