- 7,782 viewsDuration: 3:22Wabunge wanaoegemea upande wa serikali wamepuuzilia mbali madai ya kinara wa DCP, Rigathi Gachagua, kuhusu utendakazi wa Rais William Ruto katika miaka minne ya uongozi wake. Wakiongozwa na Kiongozi wa Wengi katika Bunge la Kitaifa, Kimani Ichung’wah, wabunge hao walimtaka Gachagua kuwasilisha taarifa kuhusu vifo vya watu mashuhuri vilivyotokea katika vituo vya polisi, wakidai kuwa ripoti yake ililenga kumchafua Rais Ruto kutokana na machungu ya kuondolewa afisini.