- 1,455 viewsDuration: 5:44Familia nyingi katika Kaunti ya Tana River hulazimika kuhama mara kwa mara mafuriko ya Mto Tana yanapovamia makazi yao. Hata hivyo, wakazi katika vijiji vya Kelo Kelo na Bondeni wamefanikiwa kubadilisha maisha yao kupitia mradi wa kilimo cha umwagiliaji unaotumia maji kutoka mto huo huo uliokuwa ukiwasababishia maafa na hasara kubwa. Juhudi hizo zimebadilisha mazingira yao kwa kiasi kikubwa na kuimarisha utoshelevu wa chakula katika eneo hilo.