- 254 viewsDuration: 3:06Takriban mwaka mmoja baada ya nyumba za wakazi wapatao 3,000 wa Mkocheni, eneo bunge la Taveta, Kaunti ya Taita Taveta, kubomolewa kufuatia mzozo wa ardhi, wakazi hao bado wanakabiliwa na changamoto za makazi. Familia zaidi ya 20 zimekuwa zikiishi pamoja, huku baadhi ya wanaume wakilazimika kulala kwenye mahema kwa takriban miezi tisa sasa. Julius Joho alizuru kijiji hicho na kuandaa taarifa ifuatayo.