Skip to main content
Skip to main content

Wanafunzi wa shule ya msingi ya Laramoru, Baringo, wasomea chini ya miti

  • | Citizen TV
    226 views
    Duration: 1:44
    Wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Laramoru katika eneo la Baringo Kusini sasa wanalazimika kuhudhuria masomo chini ya miti baada ya shule yao kubomolewa na maafisa wa Huduma ya Misitu ya Kenya (KFS), hali ambayo imeibua hofu kuhusu mustakabali wa elimu na amani katika eneo hilo. Shule hiyo ilikuwa na mchango mkubwa katika kuimarisha mshikamano na kuishi kwa amani kati ya jamii za Ilchamus, Pokot na Tugen, ambazo kihistoria zimekuwa na migogoro. KFS ilisema shule hiyo ilikuwa imejengwa ndani ya Msitu wa Mukutani ambao ulitangazwa rasmi kuwa msitu wa taifa mwaka 2017.