- 231 viewsDuration: 2:20Hatima ya wanafunzi wa shule ya Msingi Loramoru eneo la Marigat kaunti ya Baringo bado inasalia kwenye njiapanda baada ya shule hiyo kubomolewa na maafisa wa shirika la huduma za misitu. Wanafunzi 84 waliokuwa wakisomea shule hii sasa wakilazimika kusomea chini ya mti kwa sasa ili kuhakikisha wanamudu kuendelea na masomo. Hata hivyo, kubomolewa kwa shule hii kumeibua changamoto miongoni mwa jamii kuhusiana na mustakabali wa elimu wa watoto wao. Shule hii ilifungwa kwa zaidi ya miaka 10 miaka ya nyuma kabla ya kufunguliwa tena mwaka wa 2024. Wakazi wakitaka suluhu ya kudumu kwa udhabiti wa shule hii