- 283 viewsDuration: 2:11Ndoto ya mwanafunzi Gladys Njoki Kariuki ya kujiunga na shule ya sekondari ilikuwa karibu kuzimika, licha ya kupata alama 64 katika mtihani wa kitaifa wa KJSEA. Ingawa alipata nafasi ya kujiunga na shule ya wasichana ya State House, hali ngumu ya maisha ilimkabili kwani wazazi wake wanaotegemea kazi za kijungujiko hawakuweza kumudu karo ya shule. Hata hivyo, tumaini hilo lilirejea baada ya Gavana wa Nairobi, kupitia wakfu wake, kugharamia kikamilifu masomo yake katika shule hiyo.