Wanafunzi Zaidi ya 200 wanaotarajiwa kujiunga na gredi ya kumi na wakakosa karo katika kaunti ya Turkana, walielekea katika makao makuu ya ofisi za Elimu mjini Lodwar kaunti ya Turkana ,wakilalamika kuwa licha ya kujiwasilisha na kufanyiwa mchujo ofisini humo,wamenyimwa ufadhili wa elimu,.
Wakiongea na wanahabari mjini Lodwar,wazazi wa watoto walemavu na mayatima wamesema licha ya kuwa na watoto wenye changamoto myingi,wamenyimwa fursa ya kupata ufadhili huo wa elimu. Serikali ya Kenya kupitia mpango wa ufadhili ya Elimu scholarship ilitoa nafasi mia tano Turkana kwa wanafunzi waliozoa alama 45 kwenda juu, Lakini wazazi hawa wanadai vigezo hivyo ni vya juu, kiasi kwamba wengi wameshindwa kupata ufadhili wa masomo.