- 469 viewsDuration: 1:53Wanaharakati wa kijamii kaunti ya Taita Taveta wameitaka serikali ya kaunti hiyo kuunga mkono ujenzi wa mnara wa kuwakumbuka maaskari wa kiafrika waliofariki katika vita vya kwanza vya dunia. Hii ni baada ya serikali ya kaunti kupinga ujenzi wa mradi huo wa shilingi bilioni 40 ambao unatarajiwa kuzinduliwa rasmi juma hili.