Baada ya kuteuliwa kwa balozi Chirau Ali Mwakwere kuwa msemaji wa jamii ya mijikenda mwezi jana, wazee wa Kaya Tiwi kutoka kaunti ya Kwale wamemtaka msemaji huyo na wasemaji wengine wa jamii zote tisa za mijikenda kuweka kipaumbele suluhu ya dhuluma za ardhi kwa wakazi wa Pwani. Wakizungumza wakati wa kuadhimisha miaka 722 tangu kuasisiwa kwa Kaya Tiwi, wazee hao wanasema ardhi za kibinafsi na za umma katika eneo la Pwani zimekua zikinyakuliwa na wenyeji kukosa umiliki jambo ambalo sasa wanataka viongozi wa jamii kutia msukumo ili haki ipatikane. Aidha wanadai kua misitu ya Kaya pia imekua ikimezewa mate na mabwanyenye ambao wamekua wakiivamia na kuharibu tamaduni na turathi za jamii.