Wito umetolewa kwa taasisi za umma na watumishi wa umma kuzingatia uadilifu, uwajibikaji na kuheshimu utawala wa sheria. Wito huo ulitolewa wakati wa maadhimisho ya Siku ya Maadili Duniani yaliyoandaliwa jijini Nairobi. Waliozungumza, wakiongozwa na kaimu naibu katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma, Dkt. Gabriel Juma, pamoja na Abednego Etiang' kutoka Idara ya Uratibu wa shughuli za Serikali ya Kitaifa, walisema mageuzi endelevu katika taasisi mbalimbali yanaweza kuafikiwa tu ikiwa watumishi wa umma watatekeleza majukumu yao bila upendeleo na kwa heshima, huku wakizingatia maadili yasiyokiuka katiba.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive