Wafanyikazi wa chuo kikuu cha Moi wafutwa

  • | Citizen TV
    2,221 views

    Viongozi wa miungano ya wafanyakazi na wahadhiri wa chuo kikuu cha Moi kaunti ya Uasin Gishu, wamepigwa kalamu kwa kuendelea na mgomo. Wakiongea na runinga ya citizen Viongozi hao wameapa kuwa kamwe hawatatishika na wataendelea na mgomo huo hadi matakwa yao yote yatakapotekelezwa. Licha ya chuo hicho kufunguliwa rasmi shughuli za masomo zimelemazwa kabisa na mgomo huo.