Kongamano la COP29 | Bara Afrika lataka dola 1.3T kutengewa mabadiliko

  • | Citizen TV
    480 views

    Bara Afrika linalenga kuyarai mataifa kuwekeza dola trilioni 1.3 katika kupambana na mabadiliko ya hali ya anga kufikia mwaka wa 2030. Haya yamejiri kwenye kongamano la umoja wa mataifa kuhusu mabadiliko ya hali ya anga linaloendelea nchini Azerbaijan ambapo kenya imesisitiza kuwa matokeo yatakayoridhisha kwenye kongamano la mwaka huu ni yale yatakayohakikisha kuwa ahadi zinatekelezwa.