Mwanamke Bomba | Mtaalamu wa macho Lillian Kwamboka

  • | Citizen TV
    403 views

    Udaktari, uanasheria na uhandishi ni taalamu ambazo Watoto wengi wanapoinukia wanakuwa na ari ya kuzifanya, huku idadi ya wanawake sasa ikionekana kungozeka maradufu katika sekta hizo. Japo Lilian Kwamboka alitaka sana kusomea taaluma ya udaktari na hakutarajia kwamba angeishia kuwa mtaalamu wa upasuaji wa macho kazi ambayo ameifanya kwa miaka 15 sasa. Kupitia ukakamavu na ujasiri wake lilian amekuwa mwanamke wa kwanza na wapekee barani afrika anayefanya upasuaji wa macho kwa Watoto maafuru bag in the lens huku akiwa na rekodi ya kufanya upasuaji 102 wa macho kwa siku kwa wagonjwa wenye utandu wa macho katika hospitali ya kwale eye centre.