- 411 viewsGhana inakabiliwa na wimbi la taarifa potofu zenye madhara. Baadhi ya waandishi wa habari wana matumaini ya kukabiliana na hali hiyo kwa kutoa ripoti sahihi. Mradi wa Media Foundation for West Africa Kwaku Asante anaongoza timu ya waandishi wa habari wa kuhakiki ukweli, Fact-Check Ghana, mradi wa Media Foundation for West Africa, wenye makao yake katika mji mkuu, Accra. Timu hiyo ina kazi ngumu ya kupambana na habari potofu na upotoshaji kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vya habari vya kawaida. Asante anasema yeye na wanahabari wenzake wana kazi kubwa ya kufanya kuhusu changamoto hiyo. Kiongozi wa Timu ya Fact Check Kwaku Asante, kiongozi wa timu ya Fact Check Ghana anasema: “Kuna taarifa nyingi potofu huko nje. Ukiamka asubuhi unakuta kuna mambo mengi yanayoulizwa. Je, unaweza kuliangalia hili kwa ajili yetu? Je, hizi ni taarifa sahihi? Je, hii ni kweli? Kuna yeyote wa kutusaidia? Kisha tunafika na kusema, “ndiyo, tumeichunguza. Huu ndio ukweli. Hii si sahihi, na hii ni taarifa sahihi.” Kuhakiki ukweli, ni kazi ambayo Asante anaipenda, kwa miaka mitano iliyopita, alifanya kazi kuwajuza raia wa Ghana na taarifa sahihi. Kwaku Asante, kiongozi wa timu ya Fact-Check Ghana asema: “Inanipa furaha kubwa kujua kwamba unafanya kitu ambacho kinaleta matokeo mazuri na ushawishi wa moja kwa moja kwa watu, kwa sababu habari za uongo zinaweza kuwa na athari mbaya sana, tizama kipindi cha Covid 19 ambapo kulikuwa na mtiririko wa habari za uongo.” Ripoti ya Isaac Kaledzi, VOA, Accra, Ghana. #ghana #factcheck #factchecking #voa #uchunguzi #uhakiki #habaripotofu #accra #waandishi
Ghana yakabiliwa na wimbi la taarifa potofu zenye madhara
- 1 May 2025 - Prof. Makau Mutua has told off critics who have questioned his appointment as President William Ruto’s Senior Advisor of Constitutional Affairs.
- 1 May 2025 - US President Donald Trump said on Wednesday that Tesla boss Elon Musk could stay working for the White House as long as he wanted but understood the tycoon wanted to get back to his businesses.
- 1 May 2025 - India's human rights body said Thursday it was investigating reports more than 100 children fell sick after eating a school lunch served after a dead snake was found in the food.
- 1 May 2025 - If the next pope is from sub-Saharan Africa, he would be the first in Catholic Church history. Catholic Africans think it is a long shot, though some are cautiously optimistic that Pope Francis’ successor could be a Black cardinal from their continent.
- 1 May 2025 - A confident President William Ruto reiterated that he will not cower from taking the unpopular leadership route to secure development for Kenyans.
- 1 May 2025 - President William Ruto has fulfilled his promise to sponsor 10 vulnerable girls from each of the 17 constituencies in Nairobi County.
- 1 May 2025 - Finance Bill 2025 will support entreprise and productivity in Kenya, President William Ruto has assured.
- 1 May 2025 - Central Organisation of Trade Unions (COTU) Secretary General Francis Atwoli has called on the government to remodel the tax deductions architecture to favour Kenyan workers.
- 1 May 2025 - MP Charles Ong’ondo Were becomes the latest politician to be tragically gunned down.
- 1 May 2025 - Nine officers sustained injuries in the fight against crime in various parts of the country.