- 229 viewsKwa kuenea kwa taarifa za uongo kwenye mitandao ya kijamii, waandishi wa habari nchini Msumbiji wako mstari wa mbele katika kupambana na upotoshaji na taarifa za uongo. Hapa katika chumba cha habari cha Evidencias, mjini Maputo, Msumbiji, Reginaldo Tchambule na timu yake wanafanya kazi ya kuweka rekodi sawa katika jitihada za kupambana na upotoshaji na taarifa za uongo. Yeye na mwenzake Nelson Mucandze, wanasema walianzisha pamoja gazeti na lile la mtandaoni miaka minne iliyopita kwa sababu mashirika mengine mengi hayakuwa yakikagua ukweli au kutumia taarifa na uchambuzi katika kuripoti kwao. Tchambule anasema hadhira yao ilianza kufuatilia kwa haraka. Reginaldo Tchambule, Evidencias Editor anaeleza: “Gazeti la Evidencias linaweza kuwa limepata muonekano na umaarufu mkubwa katika muda mfupi, kwa sababu ya jinsi tulivyozingatia uandishi wa habari wenyewe. Wakati fulani tulikuwa na ukurasa ambapo tulichunguza habari kuu zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii.” Mwaka huu, Tchambule aliripoti kwa nini Ossufo Momade, kiongozi wa Renamo, chama kikuu cha upinzani cha Msumbiji, hajaonekana hadharani kwa wiki kadhaa wakati wa kampeni za urais. Evidencias ilianza kuchunguza picha kwenye mtandao wa Facebook wa mgombea ambapo ilionekana Momade alikuwa akifanya kazi nje ya nchi. Ripoti ya Amarilis Gule VOA Maputo. #habaripotofu #msumbiji #maputo #chumbachahabari #Evidencias #gazeti #reginaldotchambule #voa #voaswahili
Nchini Msumbiji waandishi waongeza juhudi kukabiliana na habari potofu
- 17 Jun 2025 - City car dealer and businessman Joseph Kairo Wambui, alias Khalif Kairo has filed an application seeking the recusal of Senior Principal Magistrate M. Murage from presiding over his ongoing criminal trial, citing alleged bias and a compromised…
- 17 Jun 2025 - Three men have been charged with the murder of Kasipul MP Charles Ong'odo Were.
- 17 Jun 2025 - Africa is not a passive recipient of aid or a battleground for influence but a continent at the threshold of intra-Africa trade and economic independence, Prime Cabinet Secretary Musalia Mudavadi has said.
- 17 Jun 2025 - Update as of June 16, 2025.
- 17 Jun 2025 - Kalonzo placed the blame on security agencies, saying they have failed in their duties.
- 17 Jun 2025 - The recommendations come against the backdrop of mixed perceptions of economic performance.
- 17 Jun 2025 - A gang has temporarily foiled a protest calling for the resignation of Deputy Inspector General Eliud Lagat.
- 17 Jun 2025 - A Kenyan fraud victim loses an estimated Ksh117,000 per incident.
- 17 Jun 2025 - The High Court has declined bail applications for three accused persons in the murder of Kasipul MP Charles Ong’ondo Were. William Imoli alias Imo, Edwin Odour Odhiambo alias Machuani, and Ebel Ochieng alias Dave Calo were charged before the Kibera High…
- 17 Jun 2025 - The High Court has declined bail applications for three accused persons in the murder of Kasipul MP Charles Ong’ondo Were. Justice Diana Kavedza ruled that the three, namely Lake Basin Development Authority officer, Ebel Ochieng alias Dave Calo, Edwin…