Waliouziwa ardhi ya Mavoko na kampuni ya saruji EAPC walalamika

  • | Citizen TV
    3,061 views

    Wakazi wanaoishi katika kipande cha ardhi walichopewa na kampuni ya Saruji ya EAPC huko Mavoko kaunti ya Machakos wameiomba serikali kuwatetea baada ya watu wengine kuvamia vipande vyao vya ardhi na kuanza kuchimba mitaro kwa ujenzi wa ukuta wa ua. Wakazi hao wanashangaa ni kwa nini hilo linatendeka ilhali walisajili ardhi zao katika zoezi lililokamilka hivi majuzi na benki ya KCB la urasimishaji mashamba . Cha kushangaza ni kwamba anayevamia mashamba yao amewekewa ulinzi mkali na maafisa wa polisi .