Wanafunzi kwenye shule zilizofungwa hawajui hatma yao

  • | Citizen TV
    490 views

    Tukisalia kwenye pilkapilka za ufunguzi wa shule kwa muhula wa kwanza, wazazi, wanafunzi na wasimamizi wa shule ambazo bado hazijakubaliwa kuwa na mabweni baada ya wizara ya elimu kuziagiza kufungwa wana wasiwasi. Wazazi sasa hawajui iwapo watalazimika kuwahamisha wana wao kwani wizara ya elimu inashikilia kuwa sharti masharti yote yaliyowekwa yatimizwe na shule hizo kukaguliwa upya kabla ya kuruhusiwa kupokea wanafunzi..