Billy Mwangi mmoja wa vijana walioripotiwa kutekwa nyara aungana tena familia yake

  • | K24 Video
    890 views

    Billy Mwangi mmoja wa vijana walioripotiwa kutekwa nyara na watu wasiojulikana ameungana tena familia yake baada ya siku kumi na tano. Mwangi alitekwa nayara Disemba 21 mwaka jana na watu waliokuwa wameficha nyuso zao katika duka moja mjini Embu. Kurejea kwake nyumbani kulipokelewa kwa furaha kubwa na familia ya kijana huyo saa mbili asubuhi kabla ya kupelekwa hospitalini na kuwekwa chini ya uangalizi wa madaktari.