Russia ndani ya Afrika, Lavrov atua Uganda leo

  • | VOA Swahili
    4,667 views
    Waziri mkuu wa Russia Sergey Lavrov amesisitiza kwamba Russia haihusiki kwa vyovyote vile na ongezeko la bei za bidhaa muhimu kote duniani, na kwamba taarifa hizo zinaenezwa na nchi za magharibi ili kueneza chuki dhidi yake. Amesema hayo akiwa Kampala, Uganda katika ziara yake ya nchi nne za Afrika. Lakini balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Marekani Stavros Lambrinidis, amepuuza ziara ya Lavrov Afrika akisema kwamba ni ya kueneza uongo. ##### Maandamano makali yakupinga uwepo wa MONUSCO imeendelea kwa siku ya pili huko Goma na Butembo vile vile kanyabayonga Kivu kasakazini. Waandamanaji wakiomba MONUSCO kuondoka. ##### Wimbi la joto kali linaloendelea kukumba nchi za Ulaya hadi hivi sasa limesababisha vifo vya karibu watu 1 700 nchini Hispania na Ureno, wakati moto mkubwa unaendelea kuteketeza misitu ya bara hilo. Nchi za Ulaya zinashuhudia kipindi kirefu cha joto kali kuwahi kutokea wakati wa msimu huu ya kiangazi na kusababisha joto kufika viwango vya juu kabisa.