Maafisa wa kliniki kuanza mgomo wao kumi na mbili usiku wa leo

  • | Citizen TV
    271 views

    Muungano wa maafisa kliniki nchini umetangaza mgomo kuanzia saa sita usiku, huku wakishutumu baraza la magavana kwa kupuuza matakwa yao. Wakiongozwa na katibu mkuu wa muungano huo George Gibore, maafisa hao pia waliishutumu serikali kuu kwa kuwatelekeza pamoja na wahudumu wengine wa afya. huku hayo yakijiri, muungano wa madaktari pia umetoa ilani ya siku 14 kwa serikali ya kaunti ya Kericho kuwa wataanza mgomo wao.