Serikali kutafuta ksh 25B kuziba pengo la USAID

  • | Citizen TV
    577 views

    Serikali sasa italazimika kutafuta takriban shilingi bilioni 25 ili kuziba pengo lililoachwa na kusitishwa kwa ufadhili wa Marekani katika sekta ya afya. Wizara ya Afya inasema kusitishwa kwa ufadhili huo kumeathiri huduma muhimu kama za kuwashughulikia wagonjwa wa HIV na utoaji chanjo, na sasa serikali imelazimika kutafuta wafadhili wengine ili kuhakikisha huduma hizi zinaendelea. pia serikali ina mipango ya kuhakikisha baadhi ya wafanyikazi waliokuwa wakigharimiwa na serikali ya Marekani wanasalia kazini.