- 6,671 viewsDuration: 1:20Baraza kuu la chama cha Jubilee limemteua waziri wa zamani Fred Matiang'i kuwa mgombea wa urais katika uchaguzi wa mwaka wa 2027 kwa tikiti ya chama hicho. Akitangaza uamuzi huo baada ya mkutano wa viongozi wakuu wa chama hicho hapa Nairobi, katibu mkuu wa chama hicho Jeremiah Kioni ametangaza kuwa Matiang'i pia ameteuliwa kuwa naibu kinara wa Jubilee.