- 374 viewsMvua kubwa inayoendelea msimu huu wa mvua za vuli za mwezi Oktoba hadi Disemba imesababisha maafa, uharibifu wa mali, mafuriko na watu kujeruhiwa katika sehemu mbalimbali nchini. Baadhi ya athari za kusikitisha zaidi ni maporomoko ya ardhi katika lokesheni ya Mukurtwo, kaunti ya Elgeyo Marakwet, Ijumaa usiku kufuatia mvua kubwa iliyonyesha.