Ngamia 7 wameibwa katika muda wa miezi sita eneo la Maungu, Taita Taveta

  • | Citizen TV
    286 views

    Baadhi ya wafugaji wa ngamia kaunti ya Taita Taveta wanakadiria hasara baada ya Ngamia saba kushambuliwa na kuuwawa na wezi chini ya kipindi cha miezi sita iliyopita katika shamba la kijamii la Saghalla huko Voi. Wafugaji hao sasa wakitoa wito kwa idara ya usalama eneo hilo kuingilia kati na kuwasaka wezi hao ambao wanazidi kuwangaisha kila mara. Kulingana nao, wezi hao wamekuwa wakichinja Ngamia hao na kuuza nyama kwenye miji ya kibiashara iliyo karibu. Tayari mshukiwa mmoja anazuiliwa katika kituo cha polisi cha Maungu .