Mazingira ya Wanyamapori

  • | Citizen TV
    33 views

    Kama njia moja ya kupunguza msongamano wa wanyapori katika mbuga ya kitaifa ya Nairobi, serikali inapanga kubomoa na kuhamisa baadhi ya viwanda katika eneo la EPZA huko Athi-river kaunti ya Machakos ili kupisha ujenzi wa njia ya wanyapori kuhama kutoka mbuga hiyo hadi eneo la Kapiti. Katibu katika wizara ya utalii sylvia Musieya anasema mpango huo unasubiri idhini ya baraza la mawaziri kabla ya kuanza kutekelezwa, akisema utasaiidia kupunguza msongamoano wa wanyapri mbugani na hivyo kuzuia migogoro ya mara kwa mara kati ya wanyapori na wakazi wanaopakana na mbuga hiyo.