'Ningependa kuwa Papa' - Trump

  • | BBC Swahili
    9,015 views
    Msikilize Rais wa Marekani Donald Trump akitania kwamba angependa kuwa papa ajaye, alipoulizwa na waandishi wa habari, akisema "hilo litakuwa chaguo langu la kwanza." Trump alitoa maoni hayo alipokuwa akiondoka Ikulu ya White House kuelekea Michigan, kufanya mkutano wa kusherehekea siku zake 100 za kwanza ofisini. Alipendekeza Kardinali Timothy Dolan, askofu mkuu wa New York, kama mrithi wa Papa Francis, akisema Dolan ni "mwema sana" #bbcswahili #marekani #donaldtrump Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw