Mzozo wa ardhi Diani

  • | Citizen TV
    217 views

    Familia moja eneo la Diani imejitokeza na kudai kuwa ndio wamiliki halali wa ardhi ya msikiti wa Kongo ya ekari 16 inayozozaniwa. Familia hiyo Inasema ilianza mchakato wa kusaka hati miliki ya ardhi hiyo mwaka wa 2005 kwa kwenda mahakamani. Miaka miwili baadaye mahakama ya Mombasa iliamuru sajili ya ardhi kuwapa cheti. Wanasema walitenga nusu ekari kwa ajili ya msikiti huo huku wakishikilia wao sio wanyakuzi wa ardhi kama ilivyodaiwa.