Kina mama-10 wachanga katika hospitali ya Mama Lucy walipiwa gharama za matibabu na wahisani

  • | KBC Video
    174 views

    Katika siku hii ya kuadhimisha siku ya kimataifa ya kina mama, kina mama-10 wachanga, walipokea pongezi kwa wingi kwa kuwaleta watoto wapya ulimwenguni. Katika hospitali ya Mama Lucy Kibaki jijini Nairobi, gharama zao za matibabu zililipwa na wahisani wakarimu na pia walitunukiwa bidhaa muhimu za wanao ili kuwasaidia kuanza safari yao ya ulezi kwa heshima. Kile kilichoanza kama siku ya kawaida kwao, punde iligeuka kuwa neema isiyotarajiwa, hali inayotukumbusha kwamba wakati mwingine, zawadi kubwa ni zile za ukarimu na upendo.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive