KIFO CHA KANG’ARA: KAUNTI YA KIAMBU LAWAMANI

  • | K24 Video
    132 views

    Serikali ya Kaunti ya Kiambu inalaumiwa kufuatia kifo cha Samuel Kang’ara, mwanaume wa miaka 32, aliyefariki baada ya kupigwa na maafisa wa kaunti wakati wa mzozo katika soko la Ngoriba, Thika. Kang’ara alifariki siku tisa baadaye katika hospitali ya Westlands Specialist na amezikwa Pwani, Njoro, Kaunti ya Nakuru.