Polisi wawanasa washukiwa wanne wa ujambazi Nairobi

  • | Citizen TV
    1,207 views

    Maafisa wa polisi jijini Nairobi wamewakamata raia watatu wa Uganda na Mkenya mmoja kwa madai ya kuhusika na visa vya uhalifu maeneo ya Nairobi na Magharibi mwa nchi. Washukiwa hao walionaswa wakiwa na bunduki tatu, wanadaiwa kuhusika na visa vya uhalifu katika mitaa ya Pangani, Eastleigh, Majengo na South C. Bunduki moja ilikuwa aina ya AK-47 iliyokuwa na risasi 30, bastola mbili zilizokuwa na risasi 20 na ambazo polisi wanachunguza kubaini iwapo zimetumiwa kwenye visa vya hivi punde vya uhalifu.