“Tunalinda Taifa au tunaharibu taswira ya Tanzania”

  • | BBC Swahili
    104,302 views
    “Tunalinda Taifa au tunaharibu taswira ya Tanzania” - Mbunge wa Kawe Dar es Salaam Tanzania, Askofu Josephat Gwajima , amekemea vikali vitendo vya utekaji vinavyoendelea nchini, akisema vinaiharibu taswira ya Tanzania kimataifa na kuvuruga mahusiano ya kidiplomasia. - Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam hapo jana, Gwajima alizungumzia juu ya tukio la kutekwa na kuuawa kwa kiongozi wa chama cha upinzani CHADEMA,Ali Kibao pamoja kutekwa kwa mwanaharakati wa CHADEMA, Mdude Nyagali ambaye hajulikani alipo kwa wiki tatu sasa. - Polisi nchini Tanzania wamekanusha kuhusika na matukio yote mawili. Hata hivyo wanasema uchunguzi wa matukio yote mawili haujakamilika. - Gwajima pia amezungumzia juu ya madhila yanayoripotiwa kuwafika wanarakati Boniface Mwangi kutoka Kenya na Agather Atuhaire kutoka Uganda walipokuwa mikononi mwa mamlaka za usalama Tanzania. - Mamlaka za Tanzania hazijazungumzia madai ya mateso na udhalilishwaji wa kijinsia ulioripotiwa na wanaharakati hao. - #bbcswahili #siasa #utekaji #tanzania#kenya #uganda #for #fypage #fy #kawe #gwajima #explorepage✨ #explorer #trending #viral #viralreels #viralreels #viralvideo Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw