Mwanaharakati wa mtandaoni Rose Njeri akamatwa

  • | Citizen TV
    6,423 views

    Maafisa wa DCI wangali wanamzuia Rose Njeri mwnaharakati akambaye anadaiwa Kukamatwa hapo jana kwa kile wanaharakati wenzake wanadai kwamba ni Kubuni mtandao italayotumika na Wakenya kuipinga mswada wa fedha mwaka wa 2025. Chama cha Mawakili nchini kupitia Rais wake Faith Odhiambo wamedai kwamba Juhudi zao kuhakikisha Njeri anawachiliwa zimeambulia patupu kwani hawajalubaliwa kumteta kama mawakili na kwamba tangu akamatwe hapo jana amenyimwa kuwachiliwa kwa dhamana. Baadhi ya Mawakili wakiongozwa na John Khaminwa walifika katika makao makuu ya DCI jioni ya leo kujaribu kumtetea Ila juhudi zao hazikufaulu. Kufikia sasa hakuna taarifa yoyote iliyotewa kuhusu sababu ya kukamatwa awake